1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BOGOTA: Kamanda wa waasi auawa Colombia

4 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBSt

Waziri wa Ulinzi wa Colombia Juan Manuel Santos amesema,wanajeshi wamemuua kamanda wa ngazi ya juu wa kundi la waasi FARC linalofuata sera kali za mrengo wa kushoto.Amesema,Tomas Medina aliuawa baada ya kambi yake msituni,kuvamiwa mwishoni mwa juma,karibu na mpaka wa Venezuela.Waziri Santos alipozungumza na waandishi wa habari alisema,kifo cha Medina ni pigo kubwa kabisa kwa miundombinu ya FARC.Medina alikuwa na dhamana kubwa ya kukusanya pesa za biashara ya madawa ya kulevya, mashariki ya Colombia.