BND lakiri kumpeleleza mwandishi habari
20 Aprili 2008Matangazo
Berlin:
Shirika la upelelezi la Ujerumani BND, linaripotiwa kukiri kwamba lilizichunguza kinyume cha sheria barua pepe za mwandishi mmoja wa kike wa habari wa kijerumani anayefanya kazi na jarida la "Der Spiegel". Kwa mujibu wa jarida hilo la kila wiki, rais wa Shirika hilo la upelelezi Ernst uhrlau alimuarifu mwandishi huyo wa habari juu ya kadhia hiyo na kumuomba radhi. Wafanyakazi wa BND wanasemekana walikua wakifuatilia mawasiliano yote ya barua pepe ya mwandishi huyo pamoja na mwanasiasa mmoja wa Afghanistan, kuanzia mwezi Juni hadi Novemba 2006.