1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken: Tumedhamiria kusitisha vita Ukanda wa Gaza

13 Juni 2024

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Anthony Blinken amesema mkataba ulio mezani wa kusitisha vita kwenye Ukanda wa Gaza bado unaweza kuafikiwa.

https://p.dw.com/p/4gyW9
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Anthony Blinken
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Anthony Blinken.Picha: Amr Nabil/AP Photo/picture alliance

Mwanadiplomasia huyo wa Marekania likuwa akizungumzawakati akihitimisha ziara yake kwenye kanda ya Mashariki ya Kati iliyonuwia kuupigia debe mkataba wa kusitisha vita uliopendekezwa na Rais Joe Biden.

Blinken ambaye jana Jumatano aliitembelea Qatar amesema watasubiri kuona iwapo tofauti zilizojitokeza kuhusu mkataba huo zitaweza kutatuliwa katika siku zinazokuja.

Mpango huo wenye hatua tatu na ambao umeidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unajumuisha usitishaji vita kwa muda wa wiki sita, kubadilishana mateka na wafungwa pamoja na mkakati wa kuujenga upya Ukanda wa Gaza.

Hata hivyo kundi la Hamas limesema baadhi ya vipengele vyake havitekelezeki na hapo jana liliwasilisha mapendekezo ya kuuboresha mpango huo. Israel nayo kwa upande wake imesema inautafakari lakini bado haijatoa jibu la mwisho.