1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Antony Blinken aaahidi msaada kwa Asia ya Kati

28 Februari 2023

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken ameahidi msaada wa Marekani kwa Asia ya Kati ili kupunguza utegemezi wa kanda hiyo kwa Urusi

https://p.dw.com/p/4O57c
US-Außenminister Antony Blinken
Picha: Burhan Ozbilici/AP/picture alliance

Siku chache baada ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu uvamizi wa Urusi, mwanadiplomasia huyo mkuu wa Marekani amekutana na wenzake kutoka mataifa yote matano ya Asia ya Kati ambako Moscow kwa muda mrefu imekuwa nguvu kubwa na sumaku kwa wafanyakazi, na ambako nchi jirani China pia ina unashiwishi unaoongezeka.

Akiwa katika mji mkuu wa Kazakhstan, Astana, Blinken ametangaza msaada wa dola milioni 25, kando na dola za awali milioni 25 zilizotangazwa Septemba, kuyasaidia mataifa ya Asia ya Kati kutanua njia za biashara na kutengeneza nafasi za kazi nyumbani.