1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken: Iran inaendelea na uundaji wa silaha za nyuklia

20 Julai 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema Iran ina uwezo wa kutengeneza nyenzo za malighafi zenye kufanikisha utengenezaji wa silaha za nyuklia ndani ya "wiki moja au mbili.

https://p.dw.com/p/4iX2O
Marekani Washington | Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq Fuad Hussein na Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq Fuad Hussein huko Washington, DC, Machi 26, 2024.Picha: Kent Nishimura/AFP/Getty Images

Habari hizo kuhusu uwezo wa Iran zinatolewa baada ya uchaguzi wa hivi karibuni uliomuingiza madarakani Rais Masoud Pezeshkian, ambae alisema lengo lake ni kuiondoa Iran katika hali ya kutengwa, na kuonesha nia ya kufufua mazungumzo ya nyuklia kati ya Iran na mataifa yenye nguvu duniani.

Blinken anasema kile wanachokishuhudia wiki iliyopita na miezi kadhaa nikitendocha Iran kuendelea na mpango wake wa nyuklia.

Mwaka 2018, Marekani ilijiondoa katika mpango wa nyuklia, ambao uliundwa katika namna ya kudhibiti mwenendo wa matumizi ya nishati ya atomik wa Iran, kwa makubaliano ya jumuiya ya kimataifa kuliondolewa taifa hilo vikwazo.