1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken awasili Korea Kusini kushiriki mkutano wa demokrasia

17 Machi 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amewasili hii leo Korea Kusini ambako atashiriki Mkutano wa kilele wa Demokrasia ulioanzishwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2021 na rais wa Marekani Joe Biden.

https://p.dw.com/p/4dokD
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony BlinkenPicha: Saul Loeb/Pool/AP/picture alliance

Mkutano huo wa siku tatu utakaowakutanisha maafisa wa serikali na wanachama wa mashirika ya kiraia, unalenga kujadili njia za kukomesha kudorora kwa demokrasia na mmomonyoko ya haki na uhuru duniani kote, unatarajiwa kuanza kesho Jumatatu mjini Seoul.

Mkutano huo umekuwa ukikosolewa kutokana na baadhi ya nchi kama Thailand na Uturuki kutoalikwa. Baada ya mkutano huo, Blinken atafanya pia ziara nchini Ufilipino, katika juhudi za Washington kuimarisha uhusiano na nchi za bara la Asia ili kukabiliana na ushawishi wa China.