1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken asisitiza mpango wa baada ya vita wa Gaza

11 Juni 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesisitiza umuhimu wa mpango baada ya vita huko Gaza katika mkutano wake wa jana Jumatatu na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

https://p.dw.com/p/4gt5u
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Blinken nchini Israel
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Blinken alipokutana na Waziri Mkuu wa Israel Netanyahu mjini Jerusalem.Picha: Amos Ben-Gershom/GPO/dpa/picture alliance

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Blinken kadhalika amesisitiza umuhimu wa kuzuia mzozo huo usisambae zaidi katika maeneo mengine. Aidha Blinken amesisitiza kwamba kusimamisha mapigano kutafungua uwezekano wa utulivu katika eneo la mpaka wa Kaskazini wa Israeli na maingiliano zaidi na mataifa mengine ya eneo hilo, pendekezo ambalo lipo mezani kwa sasa.