1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Blinken: Bado kuna utata kuelekea usitishwaji mapigano Gaza

20 Agosti 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken anasema bado yapo maswala tata na maamuzi magumu katika mpango wa kusimamisha mapigano kwenye Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4jgAi
Israel | Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alipokutana na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema Israel imekubali pendekezo la kupunguza mvutanoPicha: Chaim Zach/Israeli Government Press Office/dpa/picture alliance

Hata hivyo Blinken amesema kuwa Israel imelikubali pendekezo la kupunguza tofauti zilizopo.

Waziri Blinken ameitaka Hamas nayo ilikubali pendekezo  hilo. Waziri huyo wa Marekani leo amewasili nchini Misri na kisha atakwenda Qatar kuendeleza mazungumzo baada ya kufanya ziara nchini Israel.

Blinken amefanya ziara hiyo siku chache baada ya wapatanishi wakiwemo Marekani kuashiria matumaini juu ya kupatikana mapatano.

Wakati waziri huyo wa Marekani anafanya ziara hiyo, pana hofu juu ya kupanuka zaidi kwa mgogoro  wa Mashariki ya Kati baada ya kuuliwa kwa  makamanda wa Hezbollah. Iran inailaumu Israel kwa mauaji hayo.