1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken akutana na Abbas mjini Ramallah

10 Januari 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken ameondoka mji wa Ramallah katika Ukingo wa Magharibi baada ya kukutana na rais wa mamlaka ya ndani ya Wapalestina Mahmoud Abbas.

https://p.dw.com/p/4b5lQ
Waziri Blinken azuru Ramallah
Waziri Antony Blinken akiwa na rais wa Mamlaka ya Wapalestian Mahmoud AbbasPicha: Evelyn Hockstein/REUTERS

Abbas amemwambia Blinken kwamba Ukanda wa Gaza ni muhimu katika azma ya Wapalestina kutaka taifa lao na hautakiwi kufungiwa kutokana na vita kati ya Israel na kundi la Hamas.

Taarifa rasmi iliyochapishwa na shirika la habari la Palestina WAFA, imemnukuu rais Abbas akisema Wapalestina hawapaswi kuondolewa kutoka Gaza au eneo linalokaliwa na Israel la Ukingo wa Magharibi.

Soma pia: Blinken kukutana na Abbas baada ya kuwahimiza Waisrael kuwalinda raia wa Gaza

Abbas ametaka kuitishwe mkutano wa kimataifa wa amani kuifikisha mwisho hatua ya Israel kuikalia ardhi ya taifa la Palestina, hatua itakayosaidia kupatikana amani na usalama kwa wote. Blinken anakwenda Manama nchini Bahrain ambako atakutana na mfalme Hamad bin Isa Al Khalifa.