1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BISSAU : Guinea Bissau yapiga kura kumchaguwa Rais mpya

24 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CErD

Wapiga kura katika taifa la Afrika Magharibi la Guinea Bissau leo wamepiga kura kumchaguwa Rais mpya katika marudio ya uchaguzi yenye lengo la kukomesha miaka kadhaa ya kutokuwepo kwa utulivu katika mojawapo ya nchi maskini kabisa duniani.

Duru hii ya pili ya uchaguzi inawapambanisha marais wawili wa zamani mgombea wa chama tawala Malam Sanha dhidi ya mgombea wa kujitegemea dikteta wa zamani wa kijeshi Joao Bernado Nino Vieira.

Nino ambaye alikwenda uhamishoni baada ya kupinduliwa hapo mwaka 1999 amerudi nchini humo hapo mwezi wa April kwa shangwe kubwa ya kushiriki katika uchaguzi huo.

Uchaguzi huo unakuja siku 8 baada ya shambulio la watu wenye silaha kwa majengo ya serikali kusababisha kuuwawa kwa polisi wawili na kujeruhiwa kwa wengine kadhaa ambapo kwayo wafuasi wa Nino wameshutumiwa kuhusika nayo.

Watuhumiwa 20 wametiwa mbaroni kwa mashambulizi hayo ya Julai 16 lakini kumekuwa hakuna taarifa rasmi iliyotolewa juu ya dhamira ya shambulio lao.