1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BISSAU Awamu ya pili ya uchaguzi kufanyika nchini Guinea Bissau

23 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF10

Awamu ya pili ya upigaji kura itafanyika nchini Guinea Bissau baada ya tume ya uchaguzi kutangaza kwamba hakuna mgombea aliyeshinda kwa zaidi ya aslimia 50 ya kura katika uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita.

Malam Bacai Sanha alijipatia kura nyingi, akifuatiwa na kiongozi wa zamani wa kijeshi, Joao Bernado Vieira katika nafasi ya pili. Kumba Yala, ambaye alitimuliwa mwaka wa 2003 katika mapinduzi ya kijeshi, alikuwa wa tatu na hatagombea tena katika awamu hiyo ya pili.

Raia wengi wana matumaini kwamba kura hiyo itamaliza hali ya wasiwasi katika taifa hilo la Afrika Magharibi. Maafisa wa uchaguzi wanasema asilimia zaidi ya 80 ya wapigaji kura walijitokeza kushiriki katika uchaguzi huo. Awamu hiyo ya pili inatarajiwa kufanyika katika kipindi cha majuma matatu yajayo.