1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BioNTech: Hakuna haja ya mabadiliko kwa chanjo yetu

10 Mei 2021

Kampuni ya dawa ya Ujerumani BioNTech imesema siku ya Jumatatu kuwa chanjo yake ya Covid-19 iliyotengeza pamoja na kampuni ya Pfizer haihitaji mabadiliko yoyote kuwezesha kutoa kinga kwa aina mpya ya virusi vya corona.

https://p.dw.com/p/3tCy0
Coronavirus Symbolbild Impfstoff
Chanjo ya Virusi ya Corona ya BioNTech na Pfizer Picha: Bildagentur-online/Ohde/picture alliance

Tangazo la kampuni hiyo limetolewa pamoja na taarifa kuwa inalenga kuongeza uzalishaji wake chanjo kufidia nakisi iliyopo duniani.

"Hadi leo, hakuna ushahidi kuwa mabadiliko yanahitajika kwenye chanjo ya Covid-19 ya BioNTech kupambana na virusi vya corona vinavyojibadili maumbile" imesema sehemu ya taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo.

Hata hivyo, kampuni hiyo imesema ili kuongeza maboresho ya chanjo yake ya sasa, tayari imeanza majaribio tangu mwezi Machi.

"Lengo la utafiti huo ni kutafuta njia za kimuundo ambazo kampuni ya BioNTech na Pfizer zinaweza kutumia iwapo virusi vya SARS-CoV-2 vinajibadilisha maumbile kiasi vikahitaji mabadiliko kwenye chanjo iliyopo" imeongeza taarifa ya kampuni hiyo.

Kiwanda kingine cha BioNTech kujengwa Singapore 

Tableau | Coronavirus Chile | 24.03.21
Picha: Claudio Reyes/AFP

Tathmini ya kitabibu  pia inaendelea ili kubaini iwapo dozi ya tatu ya chanjo hiyo inaweza kuongeza uimara wa chanjo yenyewe mwili na kinga dhidi ya jamii mpya za virusi vya corona.

Katika taarifa nyingine, kampuni hiyo imesema kuwa inaanzisha kiwanda kingine cha uzalishaji nchini Singapore kutengenza mamilioni ya dozi za chanjo hiyo baadaye mwaka huu.

BioNTech yaongeza uzalishaji wa chanjo dhidi ya COVID-19

Kiwanda hicho ambacho kitakuwa cha kwanza nje ya bara la Ulaya kitakuwa sehemu ya makao makuu ya kampuni hiyo kwenye kanda ya kusini mashariki mwa bara la Asia.

Uhispania vita vya maneno vyaibuka kati ya serikali na upinzani 

Wakati hayo yakiarifiwa, nchini Uhispania, serikali na upinzani zinalaumiana baada ya kundi la vijana wengi wakiwa bila barakoa kufanya starehe kwa wingi kwenye miji ya Madrid na Barcelona mwishoni mwa juma baada ya kufikia mwisho vizuizi viliyowekwa kukabiliana na janga la corona.

Spanien, Barcelona | Nächtliche Ausgangssperre aufgehoben
Vijana wakifanya starehe huko Uhispania Picha: Jordi Boixareu/ZUMA/picture alliance

Vizuizi vilivyowekwa mwezi Oktoba baada ya kuzuka kwa wimbi kubwa la pili la maambukizi viliweka marufku kali ikiwa amri ya kzuia watu kutoka nje usiku na zuio la watu kusafiri.

Vizuizi hivyo vilifikia mwisho mwishoni mwa juma na haivikuweza kurefushwa kutokana pamoja na mambo mengine, serikali ya kisoshalisti ya waziri mkuu Pedro Sanchez isingeweza kupata wingi wa kura bungeni.

Baada ya muda wa mwisho kufika, vijana walimiminika kwa wingi mitaani mwishoni mwa wiki huku wengi wakipuuza masharti ya afya yanayoelekezwa kujikinga na Covid-19.

"Uzembe huu wa wazi wa serikali ya Sanchez unapoteza maisha ya watu" amesema Pablo Casado, kiongozi wa chama cha kihafidhina aliyeongeza kuwa upinzani unataka kutungwe sheria mpya inakayozipa nguvu serikali za majimbo kuendelea na utekelezaji wa vizuizi.

Kwa upande wake serikali imeulaumu upinzani ikiwemo kiongozi wa kihafidhina wa jimbo la Madris, Isabel Diaz Ayuso kwa kulegeza vizuizi va kupambana na Covid-19.