1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiIran

Binti wa Kiirani aliyedaiwa kushambuliwa na polisi afariki

28 Oktoba 2023

Msichana wa Kiirani, Armita Geravand amefariki dunia kiasi mwezi mmoja baada ya kudaiwa kupigwa na Polisi wa maadili ndani ya treni kwa kukiuka sheria ya uvaaji hijabu.

https://p.dw.com/p/4Y8wb
Binti wa Kiirani Armita Geravand aliyeaga dunia.

Kifo cha binti huyo mwenye miaka 16 kimeripotiwa na shirika la habari la Iran mapema hii leo. Msichana huyo aliyezirai ndani ya treni baada ya madai ya kushambuliwa, amekuwa hospitali kwa siku 28 chini ya uangalizi maalumu.

Kisa cha Geravand kiliripotiwa kwa mara ya kwanza Oktoba 3 na shirika linalofuatilia haki za jamii ya Wakurdi la Hengaw, ambalo lilisema kuwa alijeruhiwa vibaya ndani ya treni. Hata hivyo mamlaka za Iran zinaarifu kuwa binti huyo aliugua baada ya shinikizo lake la damu kushuka ghafla na zimekanusha madai ya ugomvi uliohusisha kumgusa mwili wake au wa maneno kati yake na abiria wengine.

Kisa cha Armita Geravand aliyekuwa mwanafunzi mjini Tehran kimesababisha hasira nchini Iran na kwingineko na kuibua kumbumbumbu ya binti Mahsa Amini aliyefariki dunia mikononi mwa polisi mwaka uliopita kwa madai ya kukiuka kanuni za mavazi za nchi hiyo