1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Binti mfalme wa Japan kupoteza hadhi yake

18 Mei 2017

Binti mfalme wa Japan, Mako, mjukuu wa Mfalme Akihito, atavuliwa hadhi hiyo maana ameamua kuolewa na mchumba ambaye hatoki katika familia ya kifalme

https://p.dw.com/p/2dBav
japanische Prinzessin Mako Akishino
Picha: Getty Images/AFP/K. Nogi

Mako mwenye umri wa miaka 25 ambaye ndiye binti mkubwa wa Mwanamfalme Akishino ataolewa na Kei Komura, ambaye pia ana umri wa miaka 25 na walisoma pamoja katika Chuo Kikuu.

Lakini ndoa hiyo ina madhara yake..

Kwa mujibu wa sheria za kifalme, jamaa wa kike wa familia ya kifalme hupoteza hadhi yao kama mmoja wa familia hiyo kama wataolewa na mtu asiyetoka kwenye familia ya kifalme.

Licha ya hayo, Mwanamfalme Akishino, na mkewe Kiko wametangaza kuwa na furaha na mipango ya ndoa ya binti yao. Binti mfalme Mako ni mjukuu wa kwanza kati ya wanne wa Mfalme Akihito na mkewe, Malkia Michiko, kuvikwa pete ya uchumba.

Familia ya kifalme ya Japan ndio yenye kizazi kirefu zaidi duniani, kilichoanza miaka 2,600 iliyopita.

Mwandishi: Bruce  Amani/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu