Bingwa Italia yatimuliwa
25 Juni 2010Matangazo
Mabingwa hao wa mwaka 2006 wamefungishwa virago na Slovakia baada ya kucharazwa mabao 3-2 walipokumbana hiyo jana kwenye uwanja wa Ellis Park mjini Johannesburg.
Katika mchezo mwingine wa kuamua nani atakaesonga mbele na kuingia duru ya pili ya michuano hiyo,Paraguay iliyopambana na New Zealand, imejipatia tikti ya kubakia katika michuano hiyo, licha ya pande hizo mbili kutoka uwanjani bila ya kumpachika mwenzake hata goli moja.
Na Uholanzi imeifunga Cameroon mabao 2-1 na hivyo imeingia katika duru ya pili bila ya kushindwa katika michezo yake yote mitatu.
Japan nayo hiyo jana, katika mchezo wa kufa kupona, iliikandika Denmark mabao 3-1 na hivyo imejipatia tikti ya kusonga mbele katika michuano hiyo ya Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini.