1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden, Trump watupiana lawama juu ya wahamiaji

1 Machi 2024

Rais Joe Biden wa Marekani na rais wa zamani, Donald Trump, wametumia ziara zao katika mpaka wa Marekani na Mexico siku ya Alhamis (Februari 29) kulaumiana kuhusiana na kuvuuka kwa wahamiaji kuingia nchini humo.

https://p.dw.com/p/4d3ZY
Donald Trump akihutubia kwenye jimbo la South Carolina.
Donald Trump akihutubia kwenye jimbo la South Carolina.Picha: Andrew Harnik/AP Photo/picture alliance

Wawili hao wlierushiana lawama hizo kuelekea uchaguzi wa mwezi Novemba ambapo suala la uhamiaji limeibuka kuwa hoja kuu kwa wapiga kura.

Biden, ambaye amekuwa akilitetea suala hilo katika miezi ya hivi majuzi, alikuwa katika mji wa mpakani wa Brownsville, jimboni Texas, ambako aliwakosoa wabunge wa chama cha Republican kwa kuzikataa juhudi zisizo na upendeleo za kuzifanya sheria za uhamiaji kuwa kali zaidi, baada ya Trump kuwaambia wasiupitishe muswada ambao alisema ungelimpa ushindi wa kisera Biden.

Soma zaidi: Biden, Trump kufanya ziara kinzani mpaka wa Marekani-Mexico

Trump, kwa upande wake, alikuwa na gavana wa Texas, Greg Abbott, kisha baadaye akazungumza katika bustani ya Shelby huko Eagle Pass, akitumia maneno makali kulielezea tatizo hilo la mpakani.

"Uhamiaji ni uvamizi wa Rais Biden aliouanza miaka mitatu iliyopita," alisema Trump.