1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Uchumi

Biden aidhinisha mswada wa ukomo wa deni kuwa sheria

4 Juni 2023

Rais wa Marekani Joe Biden ametia saini na kuwa sheria, mswada wa ukomo wa deni uliopitishwa na Bunge la Marekani na kuidhinishwa na Baraza la Seneti baada ya mvutano wa majuma kadhaa.

https://p.dw.com/p/4SAgs
USA Washington | Rede Joe Biden nach Ende des Schuldenstreits
Picha: Jim Watson/AFP/Getty Images

Kutiwa saini mswada huo ni hatua muhimu ambayo imezuwia janga kubwa kwa sababu bila hatua hiyo, Marekani nchi kubwa kabisa kiuchumi duniani,ingeshindwa kulipa deni lake la taifa.

Soma pia:Ahuweni yarejea Marekani baada ya Baraza la Seneti kuuidhinisha mswada kuhusu ukomo wa deni.

Zilikuwa zimebaki siku mbili tu kabla ya hapo jana rais Biden kutia saini mswada huo ulioinusuru Marekani kutumbukia kwenye mgogoro wa kiuchumi ambao ungeathiri ulimwengu mzima.

Sasa serikali ya rais Joe Biden inaweza kukopa zaidi.