1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden: Ukraine inahitaji kuendelea kusaidiwa kwa udharura

29 Novemba 2024

Rais wa Marekani Joe Biden amesema, mashambulizi ya hivi karibuni ya Urusi dhidi ya Ukraine yanaonyesha dharura ya kuiunga mkono Ukraine.

https://p.dw.com/p/4nYlf
Joe Biden
Joe Biden Picha: Saul Loeb/AFP/Getty Images

Rais wa Marekani Joe Biden amesema, mashambulizi ya hivi karibuni ya Urusi dhidi ya Ukraine yanaonyesha dharura ya kuiunga mkono Ukraine, akipigia debe uungwaji mkono mkubwa kabla ya Rais mteule Donald Trump kuchukua madaraka mwezi Januari.

Biden ameongeza kuwa usiku kucha Urusi ilifanya mashambulizi ya kutisha ya anga dhidi ya Ukraine na kwamba mamlaka ya Ukraine iliripoti kuwa Urusi ilirusha takriban makombora na droni 200 kuilenga miji na miundombinu ya nishati yake.

Rais huyo amesema hali hiyo imewasababishia raia kukosa huduma ya umeme na kuongeza kuwa mashambulizi hayo ni ya kuchukiza na yanakumbusha juu ya umuhimu wa kuwasaidia watu wa Ukraine katika kujilinda na uvamizi wa Urusi.

Biden anayetarajiwa kuongeza msaada wa Marekani kwa Ukraine katika wiki zake za mwisho katika Ikulu ya Marekani, ameongeza kuwa ujumbe wake kwa watu wa Ukraine uko wazi na ni kwamba Marekani inasimama pamoja nayo.