1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden nchini Iraq.

3 Julai 2009

Biden atakutana na viongozi wa Iraq pamoja na makamanda wa jeshi la Marekani nchini Iraq.

https://p.dw.com/p/Igfy
Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden.Picha: AP

Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden yuko nchini Iraq katika ziara ya ghafla mjini Baghdad kukutana na viongozi wa Iraq pamoja na makamanda wa jeshi la Marekani siku chache baada ya wanajeshi wa Marekani kuondoka katika miji ya Iraq.

Ziara hii inakuja huku kukiwa na tofauti kati ya Iraq na Marekani. Uongozi wa rais Barack Obama unawashinikiza viongozi wa Kurdi wale wa madhehebu ya Shia na Sunni kutatua tatizo la muda mrefu kuhusu bishara ya mafuta pamoja na la mipaka, masuala ambayo yamekwamisha maelewano ya kisiasa nchini humo.

Biden alisema kuwa ana matumani ya kupatika kwa suluhisho nchini Iraq lakini akaongeza kuwa bado kazi kubwa inahitajika kufanywa.

Biden anafanya ziara hiyo ya siku tatu baada ya rais Obama kumteua kuongoza sera za marekani nchini Iraq wakati maafisa kutoka Marekani wakipanga mikakati ya kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani kutoka Iraq itimiapo mwaka 2012.

Katika hatua za kwanza za kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani kutoka Iraq wanajeshi hao waliwakabidhi maeneo ya miji wanajeshi wa Iraq wiki hii.

Maafisa kutoka ikulu ya Marekani walisema kuwa Biden atakutana na rais wa Iraq Jalal Talabani pamoja na makamu wa rais Nuri al-Maliki

Kati ya masuala ambayo Biden anatarajiwa kujadiliana na viongozi wa Iraq ni kuhusu umihimu wa kupatika kwa mafanikio ya kisiasa, suala ambalo litachangia kuwepo kwa utulivu nchini Iraq. Hii ndio ziara ya pili inayofanywa na Biden nchini Iraq mwaka huu na ya kwanza kabisa anayofanya akiwa makamu wa rais baada ya rais Obama kufanya ziara nchini Iraq mwezi Aprili.

Irak / US-Truppenabzug
wanajeshi wa Iraq washerehekea katika eneo la Ramadi, baada ya wanajeshi wa marekani kuondoka.Picha: AP

Maafisa nchini Marekani pia walisema kuwa Biden anaweza kukutana na mwanawe wa kiume Beau Biden anayehudumu kama mwanajeshi wa Marekani nchini Iraq akiwa kwenye kikosi cha Marekani kilichopelekwa nchini Iraq mwishoni mwa mwaka uliopita.

Biden alikutana na maafisa wa ngazi ya juu wa marekani nchini Iraq baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa marekani nchini. Hii leo Biden alifanya mashauriano na kamanda wa jeshi la Marekani nchini Iraq, Jenerali Ray Odierno pamoja na balozi wa marekani nchini Iraq Christophe Hill

Afisi ya Biden ilisema kuwa wote hao walijadili kuhusu suala la hali ya usalama nchini Iraq na uwezo wa wanajeshi wa Iraq

Ikulu ya Marekani pia ilisema kuwa Biden atashirikiana na Jenerali Ray Odierno pamoja Christopher Hill huku wanajeshi wa marekani wakijiandaa kuondoka nchini Iraq mwishoni mwa mwaka 2011.

Msemaji wa ikulu ya Marekani Robert Gibbs alisema kuwa Biden atashirikiana na wa Iraq katika lengo la kumaliza tofauti za kisiasa na keleta mardhiano ambayo yanahitajika nchini Iraq.

Hata hivyo Gibbs alisema kuwa maoni yaliyotolewa na Biden wakati mmoja ya kuyatenganisha madhehebu ya Shia , Sunni na jamii ya Kurdi katika ili kuwa maeneo yaliyojisimamia hajayakuwa katika ajenda ya uongozi wa rais Obama.

Alisema kuwa jukumu kuu la Biden ni kusafiri kwenda Iraq na kufanya mikutano na wahusika wakuu katika sera za Marekani nchini Iraq. Gibbs pia alisema kuwa wanajeshi wa Marekani waliondoka kutoka miji ya Iraq kufuatia makubaliano kati ya Marekani na serikali ya Iraq.

Mwandishi :Jason Nyakundi/AFPE

Mhariri : Mohamed Abdul Rahman