1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden na Trump washutumiana katika mdahalo wa uchaguzi

28 Juni 2024

Rais wa Marekani Joe Biden na mpinzani wake wa chama cha Republican Donald Trump wameshiriki katika mdahalo wa kwanza wa wagombea urais wa uchaguzi wa mwaka 2024 katika studio za CNN huko Atlanta, Georgia..

https://p.dw.com/p/4hdAA
Marekani | Mdahalo |  Trump na  Biden
Wagombea Urais Marekani wakiwa katika mdahalo ulioandaliwa na Shirika la Habari Marekani CNN.Picha: Mike Blake/REUTERS

Mdahalo huo kando na masuala mengine, ulijikita juu ya uchumi na sera za kigeni za nchi hiyo.


Biden alianza mdahalo huo kwa kumlaumu Trump kwa kuuporomosha uchumi wa taifa hilo wakati alipokuwa madarakani.


Kiongozi huyo pia alimkosoa Trump kwa jinsi alivyoshughulikia janga la ugonjwa wa UVIKO-19 lililosababisha vifo vya maelfu ya watu nchini Marekani. 

Soma pia:Biden, Trump wakabiliana katika madahalo wa kwanza wa uchaguzi wa rais 2024


Kwa upande wake, Trump alijibu kwa kukosoa rekodi za utawala wa Biden akisema kiongozi huyo amefanya kazi duni akiwa madarakani, na kwamba amesababisha mfumuko wa bei.


Mdahalo huo ni fursa kwa wagombea wote wawili kujaribu kuelezea sera zao za kisiasa na kuwashawishi wapiga kura.