1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden kulitembelea jimbo la North Carolina

Josephat Charo
1 Oktoba 2024

Rais Joe Biden wa Marekani atayatembelea majimbo yaliyoathiriwa na kimbunga Helene baada ya maafisa kuripoti vifo zaidi ya 100 katika majimbo kadhaa kutokana na kimbunga hicho.

https://p.dw.com/p/4lGWQ
Rais wa Marekani Joe Biden, akizungumza na waandishi habari kabla kupanda ndege yake mjini Dover kurejea Washington Septemba 29, 2024.
Rais wa Marekani Joe Biden, akizungumza na waandishi habari kabla kupanda ndege yake mjini Dover kurejea Washington Septemba 29, 2024.Picha: Manuel Balce Ceneta/AP/picture alliance

Rais wa Marekani Joe Biden amesema uharibifu uliosabishwa na kimbuga Helene kilichowaua watu zaidi ya 100 kusini mashariki mwa Marekani, ulisababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

Biden alisema hayo jana Jumatatu wakati alipoulizwa na waandishi habari katika ofisi yake ya ikulu ya mjini Washington kama mabadiliko ya hali ya hewa ndiyo ya kulaumiwa kwa mkururo wa uharibifu uliosababishwa na kimbunga Helene.

Biden amesema anapanga hivi leo kulitembelea jimbo la North Carolina lililoathiriwa na kimbunga hicho baada ya kuzungumza na gavana wa jimbo hilo Roy Cooper na Mkuu wa wakala wa shirikisho unaoshughulikia hali za dharura Deanne Criswell.

Biden atashiriki mkutano na waandishi habari na kujionea uhabifu kutokea angani huko Asheville. Amesema anapanga pia kwenda Georgia na Florida haraka iwezekanavyo.