Biden awasili Finland kuhamasisha umoja ndani ya NATO
13 Julai 2023Matangazo
Biden atashiriki katika mkutano wa kilele kati ya Marekani na mataifa ya Nordic yanayozijumuisha Finland, Sweden, Denmark, Iceland na Norway.
Kabla ya kurejea Washington, Biden atafanya mazungumzo na Rais Sauli Niinisto wa Finland ambaye nchi yake ndiyo imekuwa ya hivi karibuni kujiunga na NATO.
Soma zaidi: Biden afanya mazungumzo na viongozi wa Uingereza
Sweden inatarajia pia kujiunga na muungano huo wa kijeshi baada ya Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki kuondoa hivi majuzi pingamizi yake kwa taifa hilo.
Hata hivyo, uamuzi huo utatakiwa kuidhinishwa na bunge la Ankara.
Uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine umepelekea mataifa hayo ya Nordic kubadili misimamo yao ya kijeshi kwa lengo la kujilinda na uvamizi wa Moscow.