Biden atoa tahadhari kuhusu demokrasia tete ya ulimwengu
10 Desemba 2021Mkutano huo wa siku mbili ulioanza jana unaofanyika kwa njia ya vidio unasemekana kuwa fursa kwa viongozi na watalaamu wa mashirika ya kiraia kutoka baadhi ya nchi 110 kushirikiana katika kupiga vita ufisadi na kuimarisha haki za binadamu.
Katika mkutano huo ambao unafanyika kwa utata baada ya kutotolewa mwaliko kwa mataifa ya Urusi na China, Rais Biden amesema demokrasia inakabiliwa na changamoto endelevu na zenye kutoa tahadhari duniani kote. Biden ambae ameingia madarakani Januari, huku taifa lake ligikubikwa na mgogoro mkubwa wa kisiasa katika muongo, amesema hali ilivyo ulimwengu unaelekea upande usiofaa na kuongeza kuwa demokrasia inahitaji watu mabingwa.
Marekani yaahidi kuchangia dola milioni 424 kwa ustawi wa demokrasia.
Katika mkutano huo Biden amewatolea wito viongozi wa ulimwengu kutoa ahadi madhubuti na Marekani imetoa ahadi ya kuchangia kiasi cha dola milioni 424 katika kuchangia programu za kulinda uhuru wa habari, rushwa na kuunga mkono chaguzi huru kote duniani.
Mkutano huo ambao leo hii unaingia katika siku yake ya pili na ya mwisho unafanyika kwa njia ya video kutokana na kitisho cha janga la virusi vya corona. Mkutano huo unaoratibiwa na Ikulu ya Marekani inatoa taswira ya makabiliano kati ya demokrasia na utawala wa kiimla.
Mataifa mengi washiriki yaonesha mdororo wa demokrasia
Afisa mwandamizi wa Marekani, kutoka wizara ya mambo ya nje anahusika na ulinzi wa raia na demokrasia, Uzra Zeya amesema washiriki wa mkutano huo kutoka katika maeneo yao wameonesha kuzorota hali ya kidemokrasia katika maeneo yao. Mkutano huo ulionza kwa hotuba za ufunguzi kutoka kwa Biden pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken una wawakilishi kutoka mataifa zaidi ya 100, asasi za kiraia, sekta binafsi na asasi nyingine.
Biden anashiriki mkutano huo wa aina yake katika kupigia chapuo demokrasia akikosolewa kuhusu orodha ya washiriki, pamoja na kasoro kubwa za ndani, na hasa ile ya rais wa taifa hilo aliyepita Donald Trump kutokana na jarobio lake la kushtusha la kuyapinga maotoke ya uchaguzi uliomwingiza madarakani Biden wa 2020.
Lakini pia kuna msuguano kuhusiana nani anaepashwa kuwemo katika orodha ya waalikwa na nani anastahili kuachwa. China na Urusi, mataifa ambayoBidenanayachukulia kama vinara wa utawala wa kiimla wametengwa katika mkutano huo jambo ambalo limezusha malalamiko mengi.
Katika taarifa yao ya pamoja ya mwezi uliopita balozi Anatoly Antonov wa Urusi na mwenziwe wa China Qin Gang walisema hakuna taifa lenye uwezo wa kulitolea taifa lingine mwelekeo wa namna yake ya siasa ya uongozi.
Chanzo: AFP