1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden aongeza idadi ya wakimbizi wanaoingia Marekani

4 Mei 2021

Rais Joe Biden ametangaza, baada ya kukosolewa vikali, kuwa anaongeza idadi ya juu ya wakimbizi wanaoruhusiwa kuingia Marekani mwaka huu hadi 62,500 -- kutoka idadi ya ukomo ya 15,000 iliyowekwa na mtangulizi wake Trump

https://p.dw.com/p/3svAz
Mexiko Tijuana Migranten-Konvoi erreicht US-Grenze
Picha: Reuters/E. Garrido

Mabadiliko hayo yanafuatia upinzani kutoka kwa washirika kuhusu uamuzi wa awali wa Biden wa kudumisha viwango vya enzi ya Trump.

Biden amesema katika taarifa kuwa hatua yake inafuta idadi ya chini ya kihistoria iliyowekwa na utawala wa awali ya 15,000, ambayo haikuonyesha maadili ya Marekani kama taifa linalowakiribisha na kuwasaidia wakimbizi.

Mpango huo unahusu tu wakimbizi wanaochaguliwa la mashirika ya Marekani ya usalama na intelijensia kutoka kambi za Umoja wa Mataifa kote duniani. Utawala wa Biden unakusudia kuongeza ukomo wa hadi idadi ya juu Zaidi ya wakimbizi 125,000 katika mwaka ujao wa kifedha. 

Soma pia: Marekani yaruhusu tena wakimbizi kutoka nchi 11

Marekebisho hayo yalikaribishwa haraka na Kamati ya Seneti ya Mahusiano ya Kigeni, ambayo inadhibitiwa na chama cha Biden cha Democratic. Chama cha Uhuru wa Raia nchini Marekani, ambalo ni kundi lenye nguvu la utetezi, pia limeidhinisha hatua hiyo, likisema kuwa "sifa” ya nchi hiyo ilikuwa hatarini.

Symbolbild Mexiko Geflüchtete aus afrikanischen Ländern
Tangu kuanza mwaka wa kifedha Oktoba mosi, wakimbizi 2,000 wamepewa hifadhi MarekaniPicha: AFP/O. Martinez

Trump aliwakandamiza wakimbizi kama sehemu ya sera zake za misimamo mikali za mipaka alizotumia kwenye jukwaa lake la siasa kali za uzalendo.

Biden alifanya kampeni kwa ahadi za kurejesha mitazamo ya kitamaduni Zaidi ya Marekani. Lakini akarudi nyuma baada ya serikali yake kukumbwa na matatizo katika kukabliana na ongezeko la wahamiaji wanaoingia nchini kinyume cha sheria au kudai hifadhi kwenye mpaka wa Mexico.

Katika mabadiliko mengine na sera za Trump, Biden alitangaza Aprili kuwa mgawo unapanuliwa kwa wakimbizi kutoka Amerika ya Kati, Mashariki ya Kati na Afrika, wakati pia akifungua milango kwa nchi tatu zenye idadi kubwa ya Waislamu ambazo ni Somalia, Syria na Yemen.

Soma pia: Sera ya Trump inayopiga marufuku nchi sita kuingia Marekani

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken amesema kazi inafanywa kuimarisha uwezo wa Marekani kuwashughulikia wakimbizi ili kuwakubilia wengi kadri iwekanavyo chini ya ukomo mpya. tangu mwaka wa kifedha ulianza Oktoba mosi, ni kama wakimbizi 2,000 pekee waliopewa makazi Marekani. Maandalizi ya kusafiri yanafanywa kwa ajili ya zaidi ya wakimbizi 2,000 waliotengwa na uamuzi wa rais Trump wa Oktoba 27, 2020.

Kwa tangazo hilo la jana, Ikulu ya Marekani itatumai kuwa limeyatuliza mawimbi ya kisiasa miongoni mwa Wademocrat wakati ambapo panahitajika umoja wa chama ili kuendelea na mipango mikubwa iliyopendekezwa ya fedha za matumizi ya kijamii na miundo mbinu katika mabaraza yote ya Bunge la Marekani ambayo yamegawanyika kwa katikati.    

AFP