1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Biden amuonya Netanyahu operesheni ya ardhini mji wa Rafah

7 Mei 2024

Rais Joe Biden wa Marekani amemwonya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, dhidi ya kuuvamia mji wa Rafah unaowahifadhi mamilioni ya Wapalestina waliokimbia mapigano kutoka maeneo mengine ya Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4fZBO
Rais Joe Biden wa Marekani
Rais Joe Biden wa MarekaniPicha: Adam Schultz/White House/ZUMA Wire/ZUMAPRESS/picture alliance

Kwenye mazungumzo kwa njia ya simu na Netanyahu jana Jumatatu, Rais Biden amemtaka kiongozi huyo kutoendelea na mipango yake ya kufanya operesheni kubwa ya kijeshi kwenye mji huo uliofurika watu.

Matamshi yake yanafuatia amri iliyotolewa na Israel ya kutaka watu wayahame maeneo kadhaa ya mji huo huku vikosi vya Israel vikiongeza mashambulizi ya anga.

Hata hivyo licha ya tahadhari hiyo, saa chache baada ya mazungumzo ya simu kati ya Biden na Netanyahu, Israel ilirejea tena onyo lake kwa Wapalestina ikiwataka kuondoka Rafah ikisema inajitayarisha kutuma vikosi vyake vya ardhini.