SiasaAfrika Kusini
Biden ampongeza Ramaphosa kuchaguliwa tena Afrika Kusini
15 Juni 2024Matangazo
Rais Ramaphosaalichaguliwa na bunge katika kikao chake cha kwanza kilichofanyika Ijumaa mjini Cape Town, kufuatia uchaguzi wa Mei 29, ambamo chama cha ANC kwa mara ya kwanza kilishindwa kupata wingi wa kutosha kuunda serikali kivyake, na kulazimika kutafuta washirika kutoka vyama vya upinzani.
ANC iliungana na chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance - DA, pamoja na vyama vidogo vya Inkatha Freem na vyama vingine vidogo.
Rais Biden amesema katika taarifa kwamba anatazamia kuendeleza ushirikiano kati ya Marekani na Afrika Kusini, kutanua fursa za kiuchumi, kuwekeza katika nishati safi na kuonesha kuwa demokrasia inatimiza.