Biden alenga kuimarisha ushirikiano na Vietnam
10 Septemba 2023Biden ameelekea Vietnam akitokea katika mkutano wa kilele wa G20, ambapo atakutana na kiongozi wa chama tawala cha kikomunisti cha nchi hiyo Nguyen Phu Trong, kusaini makubaliano kuhusu ushirikiano wa kina wa kimkakati.
Soma pia: Marekani na Vietnam zaazimia kujenga 'ushirika wa kimkakati'
Lengo kubwa la ziara hiyo fupi ya Biden ni kutafuta uungwaji mkono dhidi ya ushawishi wa China unaozidi kuota mizizi. Hatua hiyo ya kukuza ushirikiano ni muhimu kwa Vietnam, ambayo ina mahusiano ya kiwango cha juu na Urusi, India, Korea ya Kusini na China pekee.
Ingawa itakuwa makini isionekane kuegemea upande wowote kati ya Marekani na China, Vietnam ina wasiwasi sawa na Washington kuhusu uchokozi unaoendelea katika Bahari ya Kusini ya China inayozozaniwa. Katika ziara hiyo rais Biden pia atakutana na Rais Vo Van Thuong na Waziri Mkuu Pham Minh Chinh.