1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden aitahadharisha Israel kuhusu misaada kutofika Gaza

8 Machi 2024

Rais wa Marekani Joe Biden ameionya Israel juu ya kutumia misaada kama "sababu ya masharti" katika vita vyake dhidi ya kundi la Hamas, Biden ametoa wito wa kusitishwa mapigano mara moja huko Gaza.

https://p.dw.com/p/4dIhN
Rais Joe Biden akihutubia taifa
Rais wa Marekani Joe Biden akitoa hotuba ya Hali ya Taifa katika bunge la Marekani huko Washington, DC, Machi 7, 2024Picha: Kevin Lamarque/REUTERS

Katika hotuba yake kwa taifa la Marekani Biden alizungumzia mzozo huo uliodumu kwa miezi mitano sasa. Kiongozi huyo ameliagiza jeshi la Marekani kuongoza mpango wa dharura wa kuwasilisha misaada katika Ukanda wa Gaza kutoka baharini. Rais huyo wa Marekani ametoa hotuba hiyo wakati ambapo matumaini yanaendeleakufifia kuhusiana na makubaliano mapya ya kusitisha mapigano kabla kuanza kwa mfungo wa Ramadhani baada ya ujumbe wa Hamas uliokuwa unashiriki mazungumzo ya kusitisha vita, kuondoka huko Cairo Misri, kwa ajili ya kufanya majadiliano na wakuu wao huko Qatar.