Biden ahofia kusambaa kwa machafuko ya Mashariki ya Kati
2 Agosti 2024Matangazo
Na kuongeza kwamba kuuwawa kwa kiongozi mkuu wa Hamas nchini Iran, hakujasaidia juhudi za mazungumzo ya kusitishwa kwa vita vya Israel dhidi ya Hamas Biden amesema hapo jana alizungumza na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na kwamba kwa sasa wana msingi wa usitishwaji wa mapigano na amemtakawaziri mkuu huyo kuanza utekelezaji wake sasa. Waziri wa mambo ya kigeniwa Marekani Antony Blinken ni miongoni mwa sauti za kimataifa zinazoongezeka kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano katika siku za hivi karibuni, akisema hiyo ndiyo njia ya pekee ya kuanza kuuvunja mzunguko wa machafuko na mateso.