1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden ahimiza kupitishwa sheria ya kupiga marufuku silaha

24 Januari 2023

Rais wa Marekani Joe Biden ametoa wito kwa Bunge kuchukua hatua ya haraka ya kupiga marufuku silaha za mashambulizi.

https://p.dw.com/p/4Mdsh
USA I Präsident Joe Biden
Picha: Andrew Harnik/AP/picture alliance

Hayo ni wakati jimbo la California likiomboleza kufuatia matukio mawili makali ya ufyatuaji risasi ndani ya masaa 48.

Rais wa Marekani Joe Biden leo ametoa wito kwa Bunge kuchukua hatua ya haraka ya kupiga marufuku silaha za mashambulizi. Hayo ni wakati jimbo la California likiomboleza kufuatia matukio mawili makali ya ufyatuaji risasi ndani ya masaa 48.

Kundi la maseneta liliwasilisha upya mswada wa Kupiga Marufuku Silaha za Mashambulizi na sheria ambayo itaongeza umri wa chini ya kununua silaha za mashambulizi kuwa 21.

Biden amesema katika taarifa kuwa janga la mashambulizi ya bunduki kote Marekani linahitaji hatua kali zaidi. Mshukiwa aliyekuwa na silaha anazuiliwa na polisi kuhusiana na mauaji ya watu saba katika eneo moja la kaskazini mwa California, siku mbili tu baada ya shambulizi la ufyatuaji risasi dhidi ya watu wengi katika maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kichina karibu na Los Angeles