1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIreland

Biden aenda Ireland ya Kaskazini

11 Aprili 2023

Rais Joe Biden wa Marekani anawasili Belfast hii leo kuzindua kumbukumbu ya miaka 25 ya makubaliano ya amani ya Ireland Kaskazini.

https://p.dw.com/p/4PukR
Joe Biden Porträt Kandidatur
Picha: Kevin Dietsch/Getty Images

Biden atakaribishwa na Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak, anayelenga kuukwamua mkwamo wa kisiasa katika eneo hilo la Uingereza, huku kukiwa na mashaka ya kiusalama yanayotishia kutia kiwingu ziara hiyo.

Msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa kwenye ikulu ya White House, John Kirby, amewaambia waandishi wa habari kwamba  Biden anajali Ireland Kaskazini na ana historia ndefu ya kuunga mkono amani na ustawi wa eneo hilo.

Kesho Jumatano, atatoa hotuba katika chuo kikuu cha Ulster mjini Belfast, itakayoashiria mafanikio makubwa tangu kusainiwa kwa makubaliano hayo ya Ijumaa Kuu, mnamo mwaka 1998.