Biden aandaa msaada wa silaha wa dola mil. 725 kwa Ukraine
28 Novemba 2024Matangazo
Utawala wa Biden unajiandaa kutoa msaada wa silaha wenye thamani ya dola milioni 725 kwa Ukraine, ukijumuisha silaha za kupambana na mizinga, droni, makombora, roketi za mfumo wa HIMARS, pamoja na mabomu ya mtawanyiko na mabomu yasiyo ya kudumu ardhini.
Soma pia: Putin asema vita vya Ukraine vinachukua mkondo wa kidunia
Msaada huu unakusudia kuipiga jeki Kyiv kabla ya Biden kuondoka madarakani mwezi Januari, na unaashiria ongezeko kubwa ikilinganishwa na msaada wa hivi karibuni, ambapo Biden anapanga kutumia hadi dola bilioni 5 zilizoidhinishwa kabla ya Rais mteule Trump kuchukua madaraka.
Marekani inaitarajia Ukraine kutumia mabomu ya ardhini katika eneo lake, na msaada huo unatarajiwa kutangazwa rasmi kwa Bunge hivi karibuni.