Biashara ya Ubani Somalia iko katika tishio
Biashara hii inasababisha miti kuangamia kwavile mahitaji ya ubani yamezidi kuwa makubwa duniani.
Harufu ya thamani
Baada ya mifugo, biashara ya ubani ni chanzo kikubwa cha mapato nchini Somalia. Lakini kuvuna ubani si kazi rahisi: wavunaji lazima wapande milima ya mawe , miamba na pia huwa wanakabiliana na nyoka wenye sumu, miongoni mwa mengine.
Hatima ya wavunaji ubani
Mvunaji wa ubani Musse Ismail Hassan alijifunza taaluma hii kutoka kwa Baba yake na babu. Anakubali kuwa hii ni kazi ya hatari, lakini anasikitika yeye hana chaguo jengine. Katika picha, anaoonekana akipumzika katika pango katika korongo karibu an Gudmo, huko Somalia.
Usalama wa wavunaji
Wavunaji huvaa mavazi maalumu, lakini mavazi hayo hutengenezwa tu na nguo za nyumbani, kama vile matambara. Huvaa nguo ambazo zinazuia ubani kuganda katika ngozi zao na viatu. Ni muhimu kukumbuka kuwa Somalia inakabiliwa na ukame, pamoja na kuwa pia kuna masikini wengi.
Rangi nyingi na ukubwa
Shughuli ya kuvuna na kuuza ubani inashirikisha familia nzima. Baada ya kukusanywa wanawake huuchambua ubani mbichi kulingana na rangi na ukubwa. katika maduka Ulaya mara nyingi utakuta ubani uliokwisha chambuliwa na kupangwa kwa mujibu wa rangi: wardi, kahawia, kijivujivu au manjano. ubani hata ukishafika majimbani kazi kubwa imefanyika
Ubani wenye ubora zaidi
Madonge haya ya ubani ni sehemu ya ubani unaoitwa "maydi". Ubani huu unasemekana ndio wa hali ya juu na kwahiyo una bei ya juu pia. Mwingi husafirishwa Saudia Arabia.
Hamna muda wa kupona
Wavunaji wa ubani lazima wavunje magome ya miti ili wapate kukusanya ubani wa thamani. Lakini siku hizi kuna mahitaji makubwa ya zao hili, hili huzua tatizo la miti kutopata nafasi ya kurudi katika hali yake ya kawaida, na husababisha miti mingi kuangamia.
Kutafita hazina
Mohammed Ahmed Ali anatafuta ubani mbichi , kama wanaume wengi katika eneo hilo. Bei ya kilo moja ya ubani mbichi imepanda na hakuna anayetaka kukosa biashara hii wakati huu.
Bado kuna muda wa kuwajibika
Wavunaji wa ubani bado wanalazimika kukabiliana na hali ngumu katika mlima wa Cal Madow katika eneo la Somalia, lakini pia hali inaweza kuzidi kuwa ngumu. Wakati huku mahitaji ya biashara hii imekuwa juu na bei pia kupanda, miti pia nayo haipati muda wa kuuguza majeraha. Biashara hii haijawahi kuwa rahisi, hali ni ngumu sana kwa wanaotafuta na kuvuna ubani.
Sote tuna jukumu
Ubani mara nyingi hutumika kwa ajili ya sherehe za dini, matibabu ya magojwa ya kuambukiza, kwa manukato na pia kupunguza wasiwasi na sonona. Lakini mara nyingi watumiaji hawafikirii jinsi gani au kwa hali gani ubani unapatikana. Kujifunza juu ya upatikanaji wa ubani unaweza kusaidia kuongeza mavuno endelevu.