1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlusconi afutiwa mashitaka ya ufisadi

15 Februari 2023

Waziri wa zamani wa Italia Silvio Berlusconi amefutiwa mashitaka ya ufisadi na kuwahonga mashahidi katika kesi inayohusiana na kile kinachofahamika kama sherehe za "bunga bunga" na wasichana wadogo.

https://p.dw.com/p/4NWFO
Italien Wahlkampf, Silvio Berlusconi
Picha: Filippo Monteforte/AFP

Mahakama mjini Milan imefanya uamuzi kuwa Berlusconi mwenye umri wa miaka 86 na washitakiwa wengine 28 wengi wao wanawake hawana hatia. 

Berlusconi akanusha kula njama kumuangusha Draghi

Waendesha mashitaka walisema Berlusconi aliwalipa wanawake hao kutoa ushahidi wa uwongo katika kesi mbili za kwanza, wakati alituhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka na kukuza ukahaba wa wasichana wadogo.

Berlusconi ambaye ni mfanyabiashara na mbunge, amefutiwa mashitaka kwa kukosekana ushahidi.