BERLIN:Waziri mteule wa Ujerumani asema hali ya fedha ni ngumu nchini
29 Oktoba 2005Matangazo
Waziri wa fedha mteule wa Ujerumani bwana Peer Steinbrück amesema kwamba Ujerumani inakabiliwa na hali ngumu katika bajeti yake.Waziri Steinbrück amesema, ili kuondokana na hali hiyo dawa chungu lazima zimezwe.
Hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kiziba pengo kubwa katika bajeti ni pamoja na kupandisha kodi na kupunguza matumizi.