BERLIN:Wafanyikazi wa Deutsche bahn i kutogoma mpaka baada ya mazungumzo
10 Agosti 2007Matangazo
Shirika la Wafanyikazi wa reli linatangaza kuwa halitafanya migomo zaidi mpaka baada ya awamu ya kwanza ya mazungumzo kuhusu suala la malipo kufanyika.Mazungumzo hayo yanawaleta pamoja wawakilishi wa shirika hilo na kampuni ya treni ya kitaifa ya Deutsche Bahn.Hatua hii inatokea baada ya madereva wa treni katika miji ya Hamburg na Berlin kusitisha huduma zao kwa saa mbili wakati wa asubuhi ulio na wasafiri wengi.Wafanyikazi hao wanadai nyongeza ya asilimia 31 ya mshahara huku kampuni ya Deutsche Bahn ikikubali kutoa asilimia 4 u nusu pekee.