BERLIN.Viongozi wa G8 kukutana mwezi Juni kujadili swala la hali ya hewa
14 Februari 2007Viongozi wa Ujerumani na Uingereza wametowa mwito kwa viongozi wenzao wanachama wa kundi la nchi nane tajiri duniani la G8 kuwajibikaika zaidi katika harakati za kulinda hali ya hewa.
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema kuwa anatarajia kuwa malengo muafaka juu ya hali ya hewa yatafikiwa katika mkutano wa kilele wa nchi nane tajiri duniani G8 hapo mwezi Juni.
Baada ya mazungumzo yake na waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair mjini London, Kansela Merkel alitangaza kwamba kabla ya mkutano huo wa kilele, utafanyika kwanza mkutano wa matayarisho mwezi Mei katika mji wa Heiligendamm katika pwani ya Baltic.
Ujerumani ni mwenyekiti wa sasa wa kundi hilo la G8 na wanachama wengine wa kundi hilo la nchi tajiri duniani ni Uingereza, Marekani, Kanada, Italia, Japan, Ufaransa na Urusi.