BERLIN:umoja wa Ulaya kutilia maanani mabadiliko ya hali ya anga
1 Machi 2007Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amehutubia Bunge mjini Berlin na kusisitiza kuwa ni muhimu kwa Umoja wa Ulaya kutia juhudi zaidi ili kupambana na athari za mabadiliko y ahali ya anga.Bi Merkel alitoa wito kwa viongozi wa uMoja wa Ulaya kuidhinisha mapendekezo ya kupunguza gesi za viwanda na kuwa mfano kwa mataifa mengine ulimwenguni.
Mawaziri wa Umoja wa Ulaya mwezi jana waliazimia kupunguza gesi za viwanda kwa aslimia 20 ifikapo mwaka 2020 ili kupambana na ongezeko la viwango vya joto ulimwenguni.Suala hilo linahitaji kuidhinishwa katika mkutano wa tarehe 8 mwezi ujao mjini Brussels,Ubelgiji.
Mkutano huo wa Ubelgiji unaazimia kufanya mabadiliko ya sera za Umoja wa Ulaya kuhusu suala la athari za mabadiliko ya hali ya anga.Bi Merkel anasistiza kuwa Ujerumani itatia juhudi zaidi ili kufikia makubaliano Fulani kuhusu mazungumzo ya biashara ya Doha