1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin.Ujerumani yaidhinisha kikosi cha wanajeshi 2,400 kwenda Lebanon.

14 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDCS

Baraza la mawaziri la Ujerumani linaloongozwa na kansela Angela Merkel limeidhinisha kuwekwa kwa wanajeshi wapatao 2,400 kama sehemu ya ujumbe wa umoja wa mataifa wa kulinda amani nchini Lebanon.

Kansela Merkel ameueleza uamuzi huo kama wa kihistoria na kuongeza kuwa unaonyesha wajibu maalum wa kihistoria wa Ujerumani kwa taifa la Israel na nia yake ya kusaidia kuleta amani katika eneo hilo.

Waziri wa ulinzi Franz Joseph Jung amesema kazi ya jeshi hilo la majini itakuwa kufanya doria katika pwani ya Lebanon kusaidia kuzuwia silaha kuingizwa kinyume na sheria kwenda kwa wanamgambo wa Hizbollah.

Wanajeshi hao wamepewa mamlaka ya kutumia nguvu iwapo itakuwa muhimu. Madaraka hayo ambayo hivi sasa yanahitaji kupata baraka ya bunge, yatafikia mwisho hapo August mwakani.