1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Mkataba wa Muungano wakubaliwa na CDU

14 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEIK

Nchini Ujerumani,chama cha kihafidhina cha CDU katika mkutano wake mjini Berlin kimeidhinisha mkataba wa kuunda serikali ya muungano pamoja na chama cha Social Demokrat SPD.Wajumbe 3 tu kutoka jumla ya 116 walipiga kura za kupinga mkataba huo.Katika mkutano wa SPD mjini Karlsruhe,mkuu wa chama,Franz Münterfering na Kansela Gerhard Schroeder anaeondoka madarakani,walisisitiza kuwa mkataba wa muungano umezingatia maadili ya kijamii na demokrasi.Kwa upande mwingine mkuu wa chama cha kihafidhina cha CSU Edmund Stoiber katika mkutano wa mjini Munich,amepinga lawama zilizotolewa kuhusu makubaliano ya kuunda serikali ya muungano.Makubaliano hayo yanafungua njia ya kuundwa serikali ya muungano mkuu chini ya uongozi wa mhafidhina Bibi Angela Merkel wa CDU.Vyama vya upinzani vya FDP na Kijani vinasema huenda vikalalamika mbele ya Mahakama ya Katiba ya Ujerumani kuhusu bajeti iliyopendekezwa na serikali mpya itakayoundwa.Vyama hivyo vinasema mikopo mipya itakayochukuliwa inapindukia vitega uchumi.