1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Mazungumzo ya kodi na uchumi yaanza tena

4 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFvQ

Mazungumzo ya bunge nchini Ujerumani yameanza tena kufunguwa njia ya punguzo la kodi na mageuzi ya kiuchumi. Waziri wa fedha Hains Eichel amerudia tena onyo la serikali kwamba kushindwa kufikiwa kwa muafaka kutatowa pigo kubwa kwa uchumi. Kumekuwepo na repoti za kutatanisha katika mazungumzo hayo juu ya nafasi ya kufikiwa kwa makubaliano ambapo magazeti kadhaa yaliripoti kwamba upizani wa kihafidhina umeshupalia msimamo wao juu ya mpango wa kupunguza kodi.Gazeti la Sueddeutsche Zeitung limesema wajumbe kutoka pande zote mbili wanatagemewa kukubaliana juu ya punguzo la kama asilimia 12 mwaka ujao ili kuwasaidia wasafiri wa treni na magari wa kila siku pamoja na wamiliki wa nyumba jambo ambalo hadi sasa inaonekana kuwa ndio kikwazo kikuu katika mazungumzo hayo.