BERLIN:Madhamana wa CDU/CDU na walinzi wa Mazingira-Grüne kukutana
23 Septemba 2005Madhamana wa vyama vya kihafidhina vya CDU /CSU wanatazamiwa kukutana hii leo na walinzi wa mazingira.
Lengo la mazungumzo hayo ni kupima uwezekano wa kuundwa serikali ya muungano wa vyama vitatu wahafidhina,Waliberali wa FDP na walinzi wa Mazingira-Die Gune.
Vyombo vya habari na vyama vya kisiasa vinafuatilizia kwa makini mazungumzo hayo.
Kuna wanaopaza sauti toka pande zote mbili,wahafidina na walinzi wa mazingira,wakihoji tofauti za maoni ni kubwa kati ya pande hizi mbili kuweza kuunda serikali ya muungano wa pande tatu-iliyopewa jina humu nchini muungano wa Jamaica.
Duru ya mwanzo ya mazungumzo ilifanyika jana kati ya vigogo wawili wa kisiasa Kansela Gerhard Scroder na Angela Merkel lakini hayakufikiwa makubaliano ingawa wamekubaliana kukutana tena jumatano ijayo.
Wengi wa wataalamu wanasema kwamba suluhisho zuri kwa Ujerumani ni kuundwa kwa serikali ya muungano wa vyama vikuu viwili,SPD cha Kansela Schröder na CDU cha Angela Merkel.