BERLIN.Hapana shaka bi Angela atapambana na Kansela Schroeder kwenye uchaguzi mkuu
23 Mei 2005Matangazo
Kiongozi wa chama kikuu cha Upinzani hapa Ujerumani cha CDU Bibi Angela Merkel anatarajiwa kupambana na Kansela Gerhard Schoeder katika uchaguzi mkuu uliopendekezwa kufanyika mapema tarehe 19 Septemba.
Wanachama wengi wa chama hicho wamesema hawatarajii mtu yoyote kumkabili bi Angela katika uteuzi utakaofanyika jumatatu ijayo.
Waziri mkuu wa chama cha CDU wa jimbo la Hesse amewaambia wandishi habari mjini Berlin kwamba wamekubaliana kwenye chama kumpa bibi Merkel wadhifa wa mgombea urais wa chama chao katika uchaguzi mkuu.