1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Gharama kuhusu mageuzi ya soko la ajira kupunguzwa

4 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CELz

Vyama vikuu viwili vya kisiasa nchini Ujerumani vimekubali kupunguza takriban Euro bilioni 2 kutoka mradi uliozusha mabishano kuhusika na mageuzi ya kufanywa katika soko la ajira.Sekta itakayoathirika zaidi ni malipo yanyotolewa kwa wakosa ajira vijana na wale waliopindukia umri wa miaka 58.Mradi huo ujilikanao kwa jina la “Hartz IV” unatekelezwa tangu miaka mitatu ya nyuma katika juhudi ya kuliimaraisha soko la ajira,lakini umeshambuliwa kwa sababu umepunguza malipo ya ruzuku.Makundi makuu mawili ya kisiasa ya Social Democrats-SPD na ya kihafidhina-CDU na CSU yamekuwa yakijaribu kupata makubaliano kuhusu ajenda ya mageuzi ili vyama hivyo viweze kuunda serikali ya muungano.