1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN.Chama cha CDU chashindwa katika uchaguzi wa majimbo mawili

18 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDBC

Wanasiasa wa Ujerumani wametoa mwito wa kufanya kwa juhudi kwa ajili ya kugeuza nia za watu wanaojiunga na makundi yenye mrengo mkali wa kulia. Mwito huo umetokea baada ya uchaguzi katika majimbo mawili uliofanyika hapo jana. Katika eneo la mashariki mwa jimbo la Mecklenburg Pomerania magharibi chama cha mrengo mkali cha National Demokratik kilifanikiwa kupata viti sita vya bunge. Kiongozi wa chama SPD katika jimbo hilo bwana Till Backhaus amesema ni wajibu wa chama chake kuwaeleza watu kwamba chama cha National Demokratic hakina uwezo wa kutatua matatizio ya jimbo hilo ambalo kwa sasa linakabiliwa na ukosefu wa kazi unaofikia kiwango cha asilimia 18.

Hata hivyo cha SPD bado kitaendelea kuwa chenye nguvu kubwa katika jimbo hilo licha ya kupoteza kura kidogo. Katika mji mkuu wa Berlin chama cha SPD kilishinda huku chama cha CDU kinacho ongozwa na kansela Angela Merkel kikishindwa vibaya katika kiwango kisicho mithilika tokea kumalizika vita vikuu vya pili vya dunia. Wakati huohuo kansela Angela Merkel amesema licha ya matokeo mabaya ya chama chake cha CDU katika uchaguzi huo hakuna haja ya kubadili mwelekeo. Bibi Merkel amesema kuwa chama chake kitaendelea kushika uzi ule ule na kwamba hakuna njia mbadala.