1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Badala ya kuongeza kodi gharama zipunguzwe

5 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CELY

Katika majadiliano ya kuunda serikali mpya ya mseto nchini Ujerumani,mbali na kupandishwa Kodi ya Ongezeko la Thamani,suala la kuanzishwa kile kinachoitwa Kodi ya Utajiri lipo katika ajenda ya mdahalo.Kwa mujibu wa gazeti la Kijerumani “Bild am Sonntag” chama cha SPD kimetoa sharti kuwa ikubaliwe kuanzisha Kodi ya Utajiri kabla ya chama hicho kuweza kukubaliana na hatua ya kupandisha Kodi ya Ongezeko la Thamani.Kwa upande mwingine sekta ya uchumi nchini Ujerumani haijaridhika na majadiliano ya kuunda serikali ya muungano yanayoendelea kati ya vyama vikuu.Rais wa Chama cha Wafanya Biashara amesema,hadi hivi sasa hakuna anaeweza kusema kuwa hali ya kiuchumi inaimarika nchini Ujerumani.Kwa wakati huo huo ametoa wito kwa serikali ijayo ipunguze zaidi gharama zake badala ya kuchukua hatua za kupandisha kodi.