BERLIN: Ziara ya Dalai Lama yadhoofisha uhusiano wa Ujerumani na China
24 Septemba 2007Mazungumzo ya jana kati ya kansela Angela Merkel wa Ujerumani na kiongozi wa kidini wa Tibet Dalai Lama yamesababisha kudhoofika uhusiano kati ya Ujerumani na Jamuhuri ya umma wa China.
Serikali ya mjini Beijing imekataa kushiriki kwenye karamu ya jadi ya chai ya asubuhi iliyopangwa kuwaleta pamoja mawaziri wa mambo ya nchi za nje pembezoni mwa mkutano wa baraza kuu la umoja wa mataifa mjini New York.
Serikali kuu ya Ujerumani imesema hata hivyo inatilia maanani uhusiano mzuri kati yake na jamuhuri ya Umma wa China.
Waziri wa sheria Brigitte Zypries anajaribu kuitisha duru nyingine ya mazungumzo pamoja na maafisa wa China baada ya mazungmzo hayo kuahirishwa hapo jana mjini Munich.
China inalalamika dhidi ya kupokelewa kiongozi wa kidini wa Tibet Dalai Lama katika ofisi ya kansela Angela Merkel mjini Berlin.