1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Waziri wa zamani ahukumiwa kifungo cha nje kwa kuhusika na kashfa ya fedha.

18 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFLr

Waziri wa zamani wa mambo ya ndani nchini Ujerumani Bwana Manfred Kanther amepewa hukumu ya kifungo cha nje cha miezi 18 kwa kuhusika kwake katika chama chake kupata fedha kinyume cha sheria katika wakati wa utawala wa zamani wa serikali ya chama cha CDU. Mahakama ya kimkoa huko Wiesbaden pia imemuamuru kulipa faini ya Euro 25,000. Kanther amekiri miaka minne iliyopita kuwa katika mwaka 1983 amesaidia kuhamisha fedha ,kwenda katika benki moja nchini Uswisi kiasi cha Euro milioni 10 , kutoka katika hazina ya chama cha Christian Democrats katika jimbo la Hesse.

Fedha hizo hazikujulikana zimekwenda wapi. Kesi hiyo ya jimbo la Hesse ni sehemu ya kashfa kubwa ya chama ambayo ilipelekea kansela wa wakati huo Helmut Kohl kukiri kukipatia chama chake cha CDU fedha na kupokea Euro milioni moja ambazo hazikuonyeshwa katika mapato ya chama hicho, na hivyo kuwa ni michango iliyopokelewa kinyume na sheria.