BERLIN: Waziri wa ulinzi wa Marekani yuko mjini Berlin
25 Aprili 2007Matangazo
Waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates yuko mjini Berlin katika hatua ya mwisho ya ziara yake iliyokuwa na lengo la kuishawishi Urusi kulegeza msimamo wake dhidi ya mpango wa Marekani wa kuweka makombora ya ulinzi katika bara ulaya.
Bwana Gates atakutana na waziri wa ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung na pia waziri wa mambo ya nje Frak-walter Steinmier.
Berlin iliitolea mwito Washington kuihusisha Urusi kufuatia wasiwasi wake juu ya mpango huo wa Marekani uliolenga kuwekeza makombora 10 nchini Poland na kifaa cha rada katika Jamuhuri ya Czech.
Waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates amewasili katika mji mkuu wa Berlin akitokea Warsaw na Moscow.