BERLIN: Waziri wa ndani wa Ujerumani azusha mdahalo
15 Julai 2007Matangazo
Rais wa Ujerumani Horst Köhler,amechangia fikra zake katika mdahalo uliozuka nchini humu kuhusu mapendekezo ya waziri wa ndani juu ya njia za kupambana na ugaidi.Köhler amesema,yeye binafsi ana shaka,kwa mfano,kwamba mshukiwa ugaidi auliwe bila ya kuhukumiwa mahakamani.Ana shaka ikiwa hatua kama hiyo,inaweza kuchukuliwa kwa urahisi hivyo.
Juma lililopita,waziri wa ndani wa Ujerumani wa chama cha kihafidhina cha CDU,bwana Wolfgang Schäuble,alipendekeza kuwa mtu anaeshukiwa ugaidi auliwe.Pendekezo hilo limezusha mabishano nchini Ujerumani na ni mtihani mkubwa kwa serikali ya mseto.